ZANA ZA KUFUNDISHIA NA KUJIFUNZIA
Zana za Kujifunzia na Kufundishia
Mwalimu yeyote anapaswa kujifunza utengenezaji na matumizi ya zana, kwani ni
nyenzo muhimu sana katika kazi ya kufundisha na kujifunza.
Nini maana ya Zana za Kujifunzia na Kufundishia?
“Zana ni kitu chochote kinachopangwa na kutumika katika kuinua kiwango cha
elimu”.
Je, mwalimu anaweza kuwa Zana?
NDIYO, Mwalimu pamoja na vifaa vingine anaweza kuwa zana kwa sababu vifaa
vya kufundishia pamoja na mwalimu vimepangwa na kutayarishwa kwa
madhumuni ya kuboresha tendo la kujifunza na kufundisha.
Je, unadhani Mwanafunzi anaweza kujifunza pasi kuwa na Mwalimu?
NDIYO, Mwanafunzi anaweza kujifunza kwa kutumia zana pekee bila ya mwalimu
(Resource-based learning) lakini mwalimu atashindwa kufundisha bila ya
mwanafunzi ingawa anazo zana za kufundishia.
JIPIME
Mwalimu anaposimama mbele ya darasa na zana zake, Je, madhumuni na lengo
lake ni kuinua kiwango cha wanafunzi kujifunza au kuinua kiwango chake cha
kufundisha?
KUMBUKA
Lengo hasa la kutumia zana katika kufundisha ni kukuza na kuinua kiwango cha
kujifunza cha mwanafunzi.
Aina mbalimbali za Zana za Kujifunzia na Kufundishia
Zana za Kufundishia na Kujifunzia zimegawanyika katika makundi matano (5)
1. Vitu halisi
Kutokana na mpangilio wa piramidi, vitu halisi ni bora zaidi kwa Kufundishia kuliko
kifaa cha aina nyingine ile.
Kwa kutumia vitu halisi mwanafunzi anajifunza kwa udadisi, kuchunguza, na
kugundua. Pia vitu halisi vinampa mwanafunzi nafasi kubwa ya kujifunza kwa
vitendo na kutumia milango mingi ya fahamu kwa wakati mmoja. Katika Piramidi
vitu halisi vimewekwa kwenye kitako cha piramidi kuonesha umuhimu wa
utumiaji wa vitu halisi wakati wa kujifunza na kufundisha.
2. Bandia/Maumbo (Model)
Kwa ukosefu wa vitu halisi, maumbo/vitu bandia huchukua nafasi ya pili.
Mwanafunzi anapata kuona, kusikia, kuhisi kana kwamba anatunmia vitu halisi.
Bandia ni igizo la vitu halisi, hivyo huchangia iasi Fulani cha ukweli.
3. Televisheni, Video na Sinema
Televisheni inachangia katika kuonesha vitu kama vilivyo, kwa hali hii kuna ukweli
ndani ya televisheni. Televisheni inamwezesha mwanafunzi kusikia na kuona
matendo wakati ule ule yanapofanyika.
4. Chati, Picha, Mabango, Grafu na Ramani
Zana hizi hutoa mawasiliano ya kuona tu. Mwanafunzi anajifunza kwa kutumia
macho yake tu.
5. Radio, Santuri, Tepu-Rekoda
Zana hizi humsaidia mwanafunzi kujifunza kwa kusikia. Vipindi maalum
hutayarishwa kwa ajili ya shule au wanafunzi wanaosoma kwa masafa.
JIPIME
Toa sababu ya mpangilio wa zana za kujifunzia na kufundishia kupangwa
kwa umbo la piramidi.
Mgawanyo wa Zana za Kujifunzia na KufundishiaZana za Kujifunzia na Kufundishia zinaweza kugawanywa katika makundi makuu
mawili (2);
1. Zana za Ziada
Hizi ni aina ya zana zinazomsaidia mwalimu kuchapuza somo lake. Kwa kutumia
zana za ziada mwanafunzi hapati fursa ya kujifunza kwa vitendo yale mambo
anayojifunza, bali mwanafunzi hubaki kusikiliza tu. (mfano radio, tepu rekoda na
santuri).
2. Zana Unganishi
Hizi ni aina ya zana zenye msaada mkubwa wakati wa ufundishaji. Zanan
unganishi hazimsaidii mwanafunzi katika kujifunza tu bali zinamsaidia mwanafunzi
kufanya kwa vitendo yale anayojifunza.
(mfano vitu halisi, bandia, chati, ramani, picha, na maabara)
Ufundishaji bainifu
Ufundishaji bainifu ni nini?
ni mbinu nyumbulifu kwa ajili ya kuangalia, kuweka kumbukumbu na kutafsiri kile
ambacho wanafunzi wamejifunza kuhusu kusoma na kuandika.
Ni katika kujua kile ambacho wanafunzi wanakijua ndipo tunapokuwa na uwezo
wa kufundisha kile wanachohitaji. Walimu bora huweza na hulazimika
kuwaendeleza wanafunzi wao. Hii ina maana kuwa, walimu lazima wawe na
welewa mzuri kuhusu usomaji ni nini. Na ni lazima watambue jinsi gani wanafunzi
wanatumia mikakati hiyo.
Walimu husimama kwenye njia panda kati ya nyumbani na shuleni, kati ya
usomaji katika familia na usomaji shuleni, mwanzoni mwa safari. Mwalimu lazima
aelewe maarifa ya wanafunzi wanayoleta shuleni kutoka katika familia na jumuia
zao. Kuhusu sauti za lugha, herufi, maana ya maneno, thamani ya kusoma na kuandika na kadhalika
Aidha walimu lazima wawe na busara katika namna ya kuyatumia maarifa hayo ili
kuleta mabadiliko katika ufundishaji na ujifunzaji da
Comments
Post a Comment