NUKUU ZA SOMO LA TEHAMA MWAKA WA PILI MEI 2020


NUKUU ZA SOMO TEHAMA GRADE A2 MWAKA WA PILI



MADA YA KWANZA



MISINGI YA KUFUNDISHA NA KUJIFUNZA SOMO LA TEHAMA



1.1  MADHUMUNI YA KUJIFUNZA MADA HII



ÿ Kutaja misingi ya kufundisha TEHAMA



ÿ Kuelezea misingi ya kufundisha TEHAMA



ÿ Kufafanua faida za kufundisha na kujifunza misingi ya TEHAMA



ÿ Kutumia misingi ya TEHAMA katika kufundisha na kujifunza TEHAMA



1.2  MISINGI YA KUJIFUNZA/KUFUNDISHA TEHAMA



ÿ Ufundishaji na kujifunza ni lazima utumia muda mrefu kwa vitendo kuliko kumsikiliza



ÿ Kufundisha kwa majadiliano ili kupata mawazo zaidi/ujuzi zaidi



ÿ Kuwa na ushawishi, tumia ziara kwa wanafunzi



ÿ Tumia tathmini ya kila wakati kwa kuongeza hali ya kujifunza kwa wanafunzi



ÿ Andaa mazingira mazuri kwa wanafunzi ili waweze kueleza fikra zao bila woga



ÿ Fundisha kwa udadisi ili kuwafanya wanafunzi wajenge udadisi katika kujifunza



ÿ Wafundishe wanafunzi kwa kuzingatia mahitaji yao  



1.3  MAMBO YA KUZINGATIAKATIKA KUFUNDISHA TEHAMA



ÿ Usitoe kazi kwa wanafunzi, ambazo zinafanana na mazingira yao ya shule na nyumbani



ÿ Usiwape wanafunzi tarakirishi/kompyuta kabla ya kuandaa kazi/zoezi kwa ajili yao



ÿ Usiruhusu wanafunzi kuwa na komputa/kutumia komputa wakati unafundisha kwa mara ya kwanza/Utangulizi wa kompyuta.



ÿ Usiwaache wanafunzi katika kipindi chote wakiwa wanafanya jifunza bila kuwa kumbusha madhumuni ya somo kielimu.



ÿ Usifanye hitimisho la somo bila kufanya tafakari ya somo/mada



ÿ Usiegeme tekinolojia pekee wakati wa kufundisha



1.4  UTAWALA WA MAABARA YA KOMPYUTA



A.    Mpangilio wa Maabara ya Komputa



Maabara ya kompyuta inatakiwa iwe katika eneo ambalo walimu na wanafunzi wanaweza kutumia kompyuta kwa uraisi. Vitu vingine vya kuzingatia ni nafasi ndani ya chumba, kiwe na mwanga wa kutosha, umeme, kuwe na hewa ya kutosha na mpangilio mzuri wa kompyuta na tahadhali zake.



Katika shule, maabara ya kompyuta lazima iwe katika mpangilio ufuatao:-



Ø  Kompyuta ziwe kwa ajili ya wanafunzi na walimu



Ø  Kuwe na maabara ya kompyuta za walimu na wanafunzi



Ø  Ikiwezekana kuwe na kompyuta chache katika kila darasa

Kazi za mwalimu uonyeshwa



×  Uounysha Mbinu na mikakati ya kufundishia



×  Kuonyesha kazi za wanafunzi



×  Mbinu za kufanya tathmini kwa wanafunzi



×  Vitabu vya rejea



×  Kinasaidia kwa walimu wapya na waliokazini kwa muda mrefu



×  Kinamsaidia mwalimu kuendana na wakati katika Mbinu, maarifa na ujuzi katika kufundisha.



Ø  Ikiwezekana kuwe na kompyuta mpakato, kama vile kompyuta za mkononi ambazo zitatumika kwa kushirikiana kwa madarasa yote.



Ni muhimu maabara ya kopmyuta iwe Imeandaliwa katika mpangalio mzuri ili wanafunzi na walimu waweze kutumia kwa urahisi zaidi. Wanafunzi wanaweza kutumia kompyuta kwa ajili ya kukamilisha mazoezi yao, pia walimu wanatumia kompyuta kwa ajili ya kufundishia. Ufundishaji makini na kujifunza kwa umahiri, mambo yafuatayo lazima yazingatiwe wakati wa kuandaa maabara ya kompyuta katika shule:-



ü  Kuwe na nafasi ya kutosha katika chumba cha maabara ya kompyuta



ü  Dawati za kompyuta ziwe katika usawa wa macho



ü  Kompyuta moja itumike na wanafunzi wawili au watatu kulingana na ukubwa wa chumba cha maabara.



ü  Kuwe na printa



ü  Kuwe na vifaa vya kuprintia



ü  Kuwe na vifaa vya kuhifadhi vyaraka/data, kwa mfano Flash disk, CD-ROM



ü  Kuwe na zana zinazoendana na muhtasari ili kupunguza gharama wakati wa kufanya matengenezo



ü  Ikiwezekana kompyuta moja iwe na uwezo wa multimedia, mfano, intaneti



ü  Kuwe na netiweki ya ndani, ili iweze kusaidia kutumia printa moja kwa walimu na taasisi nzima



ü  Tumia Operating System ambayo ina Graphic User Interface-GUI



ü  Angalia Anti-virus kama haijaisha muda wake kila wakati.



Wakati unatumia maabara ya kompyuta matatizo mengi yanaweza kutokea. Matatizo haya yanaweza kama hukuzingatia mambo ya msingi wakati wa kuandaa maabara ya kompyuta. Matatizo hayo yamegawanyika katika sehemu kuu mbili, nazo ni:-



1.      Matatizo ya asili ambayo yanaweza kusababishwa na moto au umeme



2.      Matatizo yanayosababishwa na watu, kama vile vizi, mpangalio mbaya wa maabara na virusi katika kompyuta.



B.     KANUNI ZA USALAMA KATIKA MAABARA YA KOMPYUTA



Vifaa vya kompyuta vya vinavyooneka na kuweza kuvishika (Hardware) such as skrini, kibodi, kipanya (Mouse), CPU, Printa na vinginevyo, vinahitaji uangalizi wa  hali ya juu sababu ni rahisi sana kuharibika. Katika maabara ya kompyuta  usalama wa wanafunzi ni muhimu sana kuzingatia.



Kanuni na taratibu za usalama zinazotakiwa kufuatwa katika maabara ya kompyuta ni kama zifuatazo:-



v  Usiweke kompyuta katika usawa wa mwanga



v  Waya za umeme zisikatize katika maeneo ambayo wanafunzi wanapita



v  Usiweke kompyuta nyingi katika soketi moja ya umeme



v  Usiruhusu wanafunzi kurekebisha tatizo la umeme



v  CD-ROMs zinatakiwa zishikwe pembeni au kati kwenye tundu



v  Kama kompyuta haitumiki, iweke katika mpangilio mzuri na funika kwa Mifuko ya plastiki.



v  Usiondoe kompyuta kutoka sehemu moja hadi nyingine bila sababu ya msingi, kwani kopmpyuta ni raisi kuharibika kama ikiwa inaondolewa na kuhamishwa mara kwa mara.



v  Usiruhusu watumiaji wa kompyuta kuingia na chakula katika maabara ya kompyuta



v  Usiruhusu wanafunzi kukaa nyuma ya kompyuta skrini sababu kuna mionzi hatari ya x-rays.


MADA YA PILI



MAANDALIZI NA MPANGO WA KUFUNDISH TEHAMA



2.0  Utangulizi



Katika mada hii tutajifunza hatua mbalimbali za kuandaa Azimio la kazi, andaliao la somo la TEHAMA, Njia za kufundishia/kujifunzia, Maandalizi ya vifaa vya kufundishia na kujifunzia TEHAMA na Vifaa vya Mtaala vya TEHAMA.



2.1  Maana ya Vifaa vya Mtaala



Vifaa vya mtaala ni Jumla ya vifaa vyote vinavyotumika katika kusaidia na vifaa vilivyopendekezwa kutumika kwa ajili ya kuwawezesha wanafunzi wakati wa mchakato wa kufundisha na kujifunza, hivyo vinasaidia sana wanafunzi kupata maarifa kutoka katika mtaala. Vifaa vya mtaala wa TEHAMA vinahusika katika mambo yote yanayofanyika ndani ya darasa na nje ya darasa kutegemeana na sera ya elimu ya taifa.



Vifaa vya mtaala kama vile muhtasari, kiongozi cha mwalimu vinaandaliwa na Wakuzaji Mtaala (Taasisi ya Elimu Tanzania-TET). Watu Binafsi wanarusiwa kuandaa vitabu vya kiada, ziada na rejea kwa kufuata muhtasari uliopo.



2.2  Aina za Vifaa vya Mtaala



Kuna aina mbili (2) za vifaa vya Mitaala:-



1.      Vifaa vya Mtaala Vilivyoandikwa



Hivi ni vifaa vyote vilivyopo katika maandishi kama vile



·         Muhtasari wa TEHAMA



·         Vitabu vya Rejea



·         Kiongozi cha mwalimu



·         Masomo ya mtandao kama, CD-ROMs, Flash disk, Video tepu, software (website).



2.      Vifaa vya Mtaala visivyoandikwa



Kama vile



·         Kompyuta hardware, video, picha, huduma za intaneti, CD/DVD na n.k.



2.3  Kiongozi cha Mwalimu na Mwongozo wa Mwalimu



2.3.1        Kiongozi cha Mwalimu



×  Ni kitabu kinachomsaidia mwalimu kufundisha kwa mpangilio kwa kuonyesha mada na rejea za somo.



×  Ni maalum kwa mwalimu, sababu kinatoa ushauri kwa mwalimu, namna gani aweze kutumia vitabu vya kiada na ziada na namna ya kufundisha Malengo Mahsusi ya mada.



×  Kinaonyesha ujuzi katika Mbinu za kufundishia, mikakati kwa kila mada na kushauri mikakati na mbinu wakati wa tathmini.



×  Ni kizuri zaidi kwa walimu waliopo katika kazi ya ualimu kwa muda mrefu (in-service teaching).



2.3.2        Umuhimu wa Kiongozi cha Mwalimu



Kiongozi cha mwalimu kinamsaidia mwalimu kutumia muhtasari wa somo kwa umakini zaidi kwa kuzingatia mambo ya msingi yafuatayo.


×  Malengo ya somo/mada


×  Kushauri vifaa zaidi vya kujifunzia na kufundishia

Comments

Popular Posts

ZANA ZA KUFUNDISHIA NA KUJIFUNZIA

MFUMO WA MMENG'ENYO WA CHAKULA