WATANZANIA MATAJIRI DUNIANI
Takriban watanzania 435 wamekuwa mamilionea wa
dola mwaka uliopita kulingana na ripoti ya utajiri ya Knight Frank.
Waliojiunga katika klabu hiyo ya matajiri wana jumla ya thamani ya kati ya dola milioni moja hadi dola milioni 29 kila mmoja wao.
Ripoti za awali ziliwataja watanzania matajiri kama Bwana Rostam Aziz, bwana Salim Said Bakhressa, marehemu Reginald Mengi, Bw. Ally Awadh, bw. Shekhar Kanabar, Bw. Fida Hussein Rashid, Bw. Subhash Patel, bw. Yusuf Manji na bw. Salim Turky.
Kulingana na ripoti hiyo, jumla ya raia 5,553 wa Tanzania waliorodheshwa miongoni mwa watu wenye mapato ya juu mwaka uliopita, ikiwakilisha ongezeko la asilimia nane ikilinganishwa na matajiri 5,118 mwaka 2018 na 3,000 mwaka 2014.
Hatahivyo ripoti hiyo haijasema kuhusu vyanzo vya mapato hayo huku baadhi ya matajiri kutoka taifa la Kenya wakihusishwa na siasa.
Kulingana na ripoti hiyo idadi ya matajiri nchini Tanzania ilikuwa 5,668 mwisho wa mwaka 2019 ikilinganishwa na matajiri 2,942 kutoka Kenya
Hatahivyo
Inakadiriwa kwamba katika ripoti hiyo idadi ya watu binafsi waliojiunga katika ligi hiyo ya matajiri duniani itaongezeka hadi 8,532 katika kipindi cha miaka minne ijayo.
Ripoti hiyo pia inaonyesha watanzania watano walijiunga na watu walio matajiri zaidi wanaojipatia kipato kikubwa wakiwa na thamani ya dola milioni 30 juu kutoka dola milioni 999.
Katika mwaka barani Afrika 2019 Tanzania ilikuwa na matajiri 114 kati ya 302,360 ikiwa ni ongezeko la matajiri 109 mwaka 2018 na matajiri 61 2014. Idadi hiyo inatarjiwa kupanda hadi 175 kufikia 2024.
Tanzania pia ilikadiriwa kuwa nchi ya sita yenye idadi ya watu walio na mapato yenye thamani ya juu katika kipindi cha miaka mitano ijayo, nyuma ya India, Misri, Vietnam, China na Indonesia.
Kulingana na ripoti hiyo , taifa hilo la John Pombe Magufuli ndilo taifa la pekee Afrika Mashariki kuwa na bilionea wa dola za marekani ambaye ana thamani ya dola bilioni moja au zaidi.
Mtandao wa Forbes ulimtaja bilionea Mohammed Dewji ambaye anasimamia biashara ya familia kama bilionea wa dola katika eneo hili , akiwa na thamani ya dola bilioni 1.6 mwaka 2020.
Mo Dewji ambaye anasimamia kampuni ya MeTL Group ana uwekezaji katika kilimo, biashara, fedha, mawasiliano ya simu, bima, uuzaji wa nyumba, uchukuzi, mipango, pamoja na vyakula na vinywaji.
Ripoti za awali ziliwataja Watanzania matajiri kama Bwana Rostam Aziz, bwana Salim said Bakhressa, marehemu Reginald Mengi, bwana Ally Awadh, bwana Shekhar Kanabar, bwana Fida Hussein Rashid, bwana Subhash Patel, bwana Yusuf Manji na bwana Salim Turky.
Lakini utajiri wao uko chini ya dola bilioni moja.
Baadhi ya mabilionea nchini Tanzania wamewekeza nchini Kenya , Kulingana na gazeti la The standard nchini humo bilionea wa Tanzania Aunali na Sajjad rajabali waliripotiwa kununua hisa zenye thamani ya dola 70,000 katika kampuni ya Equity zenye thamani ya dola milioni 3.44 na hivyobasi kuongeza uwekezaji wake katika soka la hisa la Nairobi kufikia dpola milioniu 15.
Baadhi ya makampuni ambayo wawili hao wamewekeza fedhga zao ni pamoja na benki ya Co-oparative, Kenolkobil , Jubilee holdings na I and M Holdings.
Mbali na kenya na Tanzania , mataifa mengine ya Afrika yalioangaziwa katika ripoti hiyo ni pamoja na Botwsana , Malawi, Nigeria, Rwanda, Afrika Kusini, Uganda , Zambia na Zimbabwe.
Taifa la Afrika Kusini ndilo lililotajwa barani Afrika kuwa na mamilionea 88,460 ikifuatiwa na Nigeria ambayo ina mamilionea 40,869.
Tanzania na Kenya zaongoza kwa idadi ya mabilionea Afrika mashariki
Kenya na Tanzania zinaongoza kwa idadi ya watu matajiri katika jumuiya ya Afrika Mashariki kulingana na utafiti.
Kulingana na ripoti ya 2019 kuhusu utajiri barani Afrika iliochapishwa mwezi Septemba na benki ya AfrAsia, Kenya inaongoza ikiwa na mabilionea 356, Ikifuatiwa na Tanzania ambayo ina mabilionea 99.
Uganda ni ya tatu ikiwa na matajiri 67 huku Rwanda ikifunga orodha hiyo na mabilionea 30.
Ripoti hiyo inasema kwamba matajiri hao wana utajiri wa dola bilioni 10 na kwamba Tanzania ina tajiri mmoja wa dola bilioni moja.
Barani Afrika ripoti hiyo inasema kwamba Afrika Kusini inaongoza kwa matajiri ikiwa na mabilionea 2,169, Misri 932 na Nigeria 531.
Hatahivyo ripoti hiyo haitaji hata bilionea mmoja mbali na mali anayomiliki.
Katika miji mikuu, mji wa Nairobi unaongoza ukiwa na utajiri wa dola bilioni 49 mbele ya mji wa Dar es salaam ambao umeorodheshwa wa 11 na una utajiri wa dola bilioni 24.
Mji mkuu wa Uganda Kampala.
Comments
Post a Comment