Uraia
SEHEMU YA KWANZA: TAALUMA
1.0 DOLA
1.1 Uraia
Muda: Saa 5
1
/2
Malengo mahsusi
Baada ya kukamilisha mada ndogo hii, mwanachuo aweze:
a) Kueleza maana ya raia na dola.
b) Kutofautisha raia na somo la Uraia.
c) Kubainisha aina na sifa za Uraia.
d) Kueleza umuhimu wa somo la Uraia.
e) Kujadili umuhimu wa haki na wajibu wa raia katika dola
1.2 Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Muda: saa 5 1
/2
Malengo mahsusi.
Baada ya kukamilisha mada ndogo hii, mwanachuo aweze:
a) Kubainisha aina za katiba na sifa zake.
b) Kueleza muundo wa Katiba ya Tanzania.
c) Kujadili umuhimu wa Katiba ya Tanzania.
1.3 Bunge na Baraza la Wawakilishi Zanzibar
Muda: Saa 5 ½
Malengo mahsusi.
Baada ya kukamilisha mada ndogo hii, mwanachuo aweze:
a) Kutoafutisha Bunge la Muungano na Baraza la Wawakilishi Zanzibar.
b) Kueleza muundo wa Bunge la Muungano na Baraza la Wawakilishi la Zanzibar.
c) Kuchambua shughuli za Bunge la Muungano na Baraza la Wawakilishi la Zanzibar.
d) Kuchambua nafasi/majukumu ya chama tawala na vyama vya upinzani katika bunge, na baraza la wawakilishi la zanzibar
MAHAKAMA
Muda: saa 5 ½
Malengo mahsusi
Baada ya kukamilisha mada ndogo hii, mwanachuo aweze:
a) Kutofautisha mfumo na muundo wa Mahakama ya Tanzania na ule wa Tanzania
Zanzibar.
b) Kuainisha shughuli za Mahakama ya Tanzania na Tanzania Zanzibar.
c) Kujadili maana na umuhimu wa uhuru wa mahakama.
1.5 Serikali/Nguzo ya Utendaji
Muda: saa 5 ½
Malengo mahsusi
Baada ya kukamilisha mada ndogo hii, mwanachuo aweze:-
a) Kueleza muundo wa Serikali ya Tanzania (Nguzo ya utendaji).
b) Kuainisha kazi za Nguzo ya utendaji na viongozi wakuu katika sehemu hiyo.
c) Kutofautisha na kulinganisha shughuli za Serikali ya Muungano na zile za Serikali
ya Mapinduzi Zanzibar.
1.6 Serikali za Mitaa
Muda saa: 5 ½
Malengo mahsusi
Baada ya kukamilisha mada ndogo hii, mwanachuo aweze:
a) Kueleza muundo na majukumu ya serikali za mitaa.
b) Kufafanua vyanzo na matumizi ya mapato ya serikali za mitaa.
c) Kujadili umuhimu wa serikali za mitaa kwa maendeleo ya jamii.
d) Kujadili umuhimu na namna ya ushiriki wa raia katika serikali za mitaa
Utawala wa Kidemokrasia
Muda saa 5 ½
Malengo mahsusi.
Baada ya kukamilisha mada ndogo hii, mwanachuo aweze:
a) Kueleza maana ya demokrasia.
b) Kuchambua misingi ya Demokrasia.
c) Kueleza umuhimu wa mgawanyo wa madaraka katika utawala wa kidemokrasia.
d) Kubainisha vikwazo dhidi ya utawala wa kidemokrasia.
e) Kujadili umuhimu wa ushindani wa kidemokrasia katika siasa ya vyama vingi.
f) Kujadili jinsi rushwa inavyoathiri utawala bora na haki za binadamu hapa Tanzania
2.0 UTAMADUNI WETU
2.1 Nyanja za Utamaduni
Muda saa 5 ½
Malengo mahsusi
Baada ya kukamilisha mada ndogo hii, mwanachuo aweze:
a) Kufasiri neno utamaduni.
b) Kuainisha nyanja mbalimbali za utamaduni.
c) Kujadili umuhimu wa kila nyanja ya utamaduni na utamaduni kwa jumla.
d) Kujadili mila na desturi zinazochangia ueneaji wa masuala kama UKIMWI na
ubaguzi wa kijinsia na ukiukwaji wa haki za binadamu.
2.2 Masuala kuhusu maisha ya familia
Muda saa 5 ½
Malengo mahsusi
Baada ya kukamilisha mada ndogo hii, mwanachuo aweze:
a) Kueleza maana, aina na umuhimu wa familia.
b) Kubainisha masuala ya kijinsia katika maisha ya familia.
c) Kubainisha mila na desturi zinazoathiri ustawi wa familia.
d) Kujadili athari za ukiukwaji wa haki na wajibu wa wanafamilia.

Maadili
Muda saa 5 ½
Malengo mahsusi
Baada ya kukamilisha mada ndogo hii, mwanachuo aweze:
a) Kueleza maana, mifano na umuhimu wa maadili.
b) Kubainisha mambo yanayosababisha na kudhihirisha uwepo wa mmomonyoko wa
maadili katika jamii.
c) Kujadili athari za mmomonyoko wa maadili katika jamii.
d) Kujadili mbinu za kurekebisha na kudumisha maadili katika jamii.
2.4 Kazi
Muda saa 5 ½
Malengo mahsusi
Baada ya kukamilisha mada ndogo hii, mwanachuo aweze:
a) Kueleza maana, aina na umuhimu wa kazi kwa binadamu, hasa kwa jamii ya
Tanzania.
b) Kujadili viashiria na umuhimu wa uwajibikaji katika kazi.
c) Kubainisha mambo yanayoathiri utendaji kazi.
d) Kufafanua umuhimu wa kila mtu kufanya kazi kwa bidii na uadilifu.
2.5 Utamaduni wa Kigeni
Muda saa 5 ½
Malengo mahsusi
Baada ya kukamilisha mada ndogo hii, mwanachuo aweze:
a) Kujadili mifano na athari za utamaduni wa kigeni kwa Tanzania.
b) Kueleza jinsi sayansi na teknolojia vinavyoathiri mila na desturi za Watanzania.
c) Kuonesha umuhimu wa jamii kuwa macho na utamaduni wa kigeni
UCHUMI WA TANZANIA
Nyanja za uchumi wa Tanzania
Muda saa 5 ½
Malengo mahsusi
Baada ya kukamilisha mada ndogo hii, mwanachuo aweze:
a) Kueleza maana na umuhimu wa uchumi kwa Tanzania.
b) Kuchambua nyanja mbalimbali za uchumi.
c) Kujadili umuhimu wa nyanja mbalimbali za uchumi kwa uchumi wa Tanzania.
3.2 Mambo yanayochangia kukua au kuporomoka kwa uchumi.
Muda saa 5 ½
Malengo mahsusi
Baada ya kukamilisha mada ndogo hii, mwanachuo aweze:
a) Kubainisha mambo yanayochangia uchumi kukua au kuporomoka.
b) Kueleza umuhimu wa elimu, utaalamu, teknolojia, ujasiriamali, uongozi bora, mitaji,
bidii ya kazi, njia bora za uchukuzi, masoko, amani na utulivu na afya ya watu, katika
kukuza uchumi.
c) Kujadili umuhimu wa kutunza mazingira kwa uchumi endelevu.
3.2 Uchumi wa Soko Huria
Muda saa 5 ½
Malengo mahsusi
Baada ya kukamilisha mada ndogo hii, mwanachuo aweze:
a) Kueleza maana ya uchumi wa soko huria.
b) Kubainisha vigezo vya uchumi wa soko huria.
c) Kueleza nafasi ya Tanzania katika uchumi wa soko huria.
d) Kujadili athari za uchumi wa soko huria kwa Tanzania.
e) Kutoa mapendekezo ya namna ya kukwamua uchumi wa Tanzania.
UHUSIANO WA KIMATAIFA
4.1 Misingi inayoongoza uhusiano wa Tanzania na nchi nyingine.
Muda: saa 5 ½
Malengo mahsusi
Baada ya kukamilisha mada ndogo hii, mwanachuo aweze:
a) Kueleza maana ya uhusiano wa Kimataifa na umuhimu wake.
b) Kujadili misingi inayoongoza uhusiano wa Tanzania na mataifa mengine.
c) Kubainisha athari za misingi hiyo kwa Tanzania.
4.2 Maeneo ya Mahusiano ya Kimataifa.
Muda saa 5 ½
Malengo mahsusi
Baada ya kukamilisha mada ndogo hii, mwanachuo aweze:
a) Kueleza jinsi Tanzania inavyohusiana na mataifa mengine kijamii.
b) Kubainisha nyanja za mahusiano ya kiuchumi kati ya Tanzania na mataifa mengine.
c) Kuonesha jinsi Tanzania inavyohusiana na mataifa mengine kisiasa.
d) Kutathmini ushirikiano wa Tanzania na mataifa mengine kijamii, kiuchumi na
kisiasa.
4.3 Utandawazi
Muda saa 5 ½
Malengo mahsusi
Baada ya kukamilisha mada ndogo hii, mwanachuo aweze:
a) Kueleza maana ya utandawazi.
b) Kuchambua viashiria vya utandawazi.
c) Kujadili athari za utandawazi katika maendeleo ya Tanzania.
d) Kubainisha mikakati na changamoto za kukabiliana na athari za utandawazi.
SEHEMU YA PILI: UFUNDISHAJI
MISINGI YA UFUNDISHAJI WA SOMO LA URAIA
1.1 Ufundishaji unaozingatia ujenzi wa stadi na ujuzi wa kiraia.
Muda: saa 7
Malengo mahsusi
Baada ya kukamilisha mada ndogo hii, mwanachuo aweze:
a) Kueleza dhana ya stadi/ ujuzi wa kiraia
b) Kujadili umuhimu wa kujenga stadi na ujuzi wa kiraia.
c) Kubainisha mambo ya kuzingatia katika kufundisha stadi/ujuzi wa kiraia
d) Kufanya onyesho mbinu juu ya uchopekwaji wa ujenzi wa stadi na ujuzi wa kiraia.
e) Maswali na majibu kuhusu dhana ya stadi/ujuzi wa kiraia.
1.2 Uchanganuzi wa masuala chanya na hasi ya serikali/siasa.
Muda: saa 7
Malengo mahsusi
Baada ya kukamilisha mada ndogo hii, mwanachuo aweze:
a) Kubaini masuala chanya na hasi ya serikali/siasa
b) Kufafanua umuhimu wa kuwawezesha wanafunzi kuchanganua
c) masuala chanya na hasi ya serikali /siasa.
d) Kueleza mambo ya kuzingatia katika kufundisha wanafunzi
e) kuchanganua masuala chanya na hasi ya serikali/siasa.
f) Kufanya mazoezi ya kuchanganua masuala ya serikali na siasa.
1.3 Uhusishi wa dhana tata na uzoefu wa mwanafunzi.
Muda: saa 7
Malengo mahsusi
Baada ya kukamilisha mada ndogo hii, mwanachuo aweze:
a) Kubainisha dhana tata zilizopo kwenye somo la Uraia.
b) Kuhusisha dhana zinazofundishwa na uzoefu wa mwanafunzi
c) Kueleza mambo tata muhimu ya kuzingatia katika kuhusisha dhana tata na uzoefu
wa wanafunzi.
d) Kufanya mazoezi ya kuhusisha dhana tata na uzoefu wa wanafunzi kufundisha somo la uraia
e) kuchambu kitabu cha kiada
Uhusishi wa mada za Uraia na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Muda saa 7
Malengo mahsusi
Baada ya kukamilisha mada ndogo hii mwanachuo aweze:
a) Kubaini vipengele vya Katiba vyenye uhusiano na mada mbalimbali za somo Uraia.
b) Kubainisha mambo ya kuzingatia katika kuhusisha Katiba na mada inayofundishwa
c) Kufanya mazoezi mbalimbali ya kuhusisha mada mbalimbali na vipengele muhimu
vya Katiba
2.0 UCHAMBUZI WA MAANDIKO/MACHAPISHO MUHIMU YA KUFUNDISHIA
/KUJIFUNZIA SOMO LA URAIA
2.1 Uchambuzi wa Muhtasari
Muda saa 7
Baada ya kukamilisha mada ndogo hii, mwanachuo aweze:
a) Kueleza maana ya muhtasari.
b) Kuchambua vipengele vikuu vya muhtasari wa somo la Uraia.
c) Kueleza sifa za muhtasari sanifu.
d) Kuchambua muhtasari wa somo la Uraia.
2.2 Uchambuzi wa kitabu cha kiada
Muda: saa 7
Malengo mahsusi
Baada ya kukamilisha mada ndogo hii, mwanachuo aweze:
a) Kubainisha sifa za kitabu cha kiada.
b) Kueleza mambo ya kuzingatia katika kutumia kitabu cha kiada.
c) Kujadili faida na matatizo ya uwepo wa vitabu vya kiada kadhaa kwa ajili ya somo la uraia
Upatikanaji wa Zana
Muda saa 8
Malengo mahsusi
Baada ya kukamilisha mada ndogo hii, mwanachuo aweze:
a) Kueleza umuhimu wa kutumia zana katika kufundishia somo la Uraia.
b) Kueleza mbinu za kupata zana za kufundishia/kujifunzia somo la Uraia.
c) Kuandaa zana za kufundishia somo la Uraia kwa kufaragua na kutengeneza.
d) Kufanya majaribio ya kufundisha kwa kutumia zana zilizoandaliwa.
3.3 Matumizi na utunzaji wa zana za kufundishia na kujifunzia
Muda saa 7
Malengo mahsusi
Baada ya kukamilisha mada ndogo hii, mwanachuo aweze:
a) Kueleza umuhimu wa kutumia zana sahihi na kwa usahihi kufundishia na
kujifunzia somo la Uraia.
b) Kutunza zana za kufundishia na kujifunzia somo.
c) Kueleza mambo ya kuzingatia wakati wa kutumia zana wakati wa ufundishaji na
ujifunzaji somo la Uraia na njia bora za kuzihifadhi, zana
d) Kueleza namna na umuhimu wa kutunza zana.
4.0 MAANDALIZI YA KUFUNDISHA SOMO LA URAIA
4.1 Kuandaa maazimio ya kazi
Muda saa 7
Malengo mahsusi
Baada ya kukamilisha mada ndogo hii, mwanachuo aweze:
a) Kueleza maana na umuhimu wa azimio la kazi
b) kufafanua vipengele vya Azimio la kazi
Kuandaa mfano wa azimio la kazi kwa kutumia mihtasari wa Uraia shule za
Msingi.
4.2 Kuandaa andalio la somo
Muda saa: 7
Malengo mahsusi
Baada ya kukamilisha mada ndogo hii, mwanachuo aweze:
a) Kueleza maana na umuhimu wa andalio la somo
b) Kufafanua vipengele vya andalio la somo
c) Kuandaa mfano wa andalio la somo kwa kutumia vifaa husika.
d) Kueleza uhusiano kati ya azimio la kazi na andalio la somo.
4.3 Kuandaa nukuu za somo na shajala
Muda saa: 2
Malengo mahsusi
Baada ya kukamilisha mada ndogo hii, mwanachuo aweze:
a) Kueleza maana na umuhimu wa nukuu za somo na shajala
b) Kufafanua mambo ya kuzingatia katika kuandaa nukuu za somo
c) Kuandaa mfano wa nukuu za somo la Uraia na shajala la kueleza namna ya
kutumia vitu hivi.
5.0 UPIMAJI NA TATHMINI
5.1 Dhana ya upimaji katika somo la Uraia.
Muda saa 7
Malengo mahsusi
Baada ya kukamilisha mada ndogo hii, mwanachuo aweze:-
a) Kueleza maana ya upimaji katika somo la Uraia
b) Kufafanua umuhimu wa upimaji katika somo la Uraia
c) Kubainisha mambo ya kuzingatia katika upimaji wa somo la Uraia.
Zana za Upimaji katika somo la Uraia.
Muda: saa 7
Malengo mahsusi
Baada ya kukamilisha mada ndogo hii, mwanachuo aweze:
a) Kubainisha zana zinazokidhi upimaji wa somo la Uraia.
b) Kutunga maswali ya upimaji kwa kuzingatia jedwali la utahini.
c) Kuandaa mwongozo wa usahishaji.
5.3 Tathmini katika somo la Uraia.
Muda: saa 7
Malengo mahsusi
Baada ya kukamilisha mada ndogo hii, mwanachuo aweze:
a) Kueleza maana na madhumuni ya tathmini katika somo la Uraia
b) Kuainisha mambo muhimu ya kuzingati wakati wa kufanya tathmini
c) Kubainisha aina za tathmini.
d) Kufafanua matumizi ya alama za mazoezi,majaribio na mitihani katika
kuboresha ufundishaji wa somo la Uraia
5.4 Maandalizi ya Ufundishaji wa Muda Mrefu
Muda saa: 1
Malengo mahsusi
Baada ya kukamilisha mada ndogo hii, mwanachuo aweze:-
a) Kueleza maandalizi yanayotakiwa ya ufundishaji wa muda mrefu.
b) Kuandaa vifaa/zana muhimu zinazohitajika kwa ajili ya ufundishaji wa muda
mrefu.
c) Kueleza umuhimu wa kuchunga mwenendo wake wakati wote atakapokuwa katika ufundishaji wa muda mrefu
REJEA ZILIZOTUMIKA
Institute of Curriculum Development (1993). A guide for Secondary School Teachers. Ecoprint
Ltd.
Institute of Curriculum Development (1993) General Studies for Advanced level (Form V – Vi)
Ecopringit Ltd.
Ministry of Education and Vocational Training (2007) Development Studies syllabus Diploma
in Secondary Education. Tanzania Institute of Education.
Ministry of Education and Vocational Training (2006) Civics syllabus for Primary School.
Tanzania Institute of Education.
Ministry of Education and Vocational Training (2005) Civics syllabus for Secondary Schools
Form I-IV institute of education
By sir Erick Gration
Comments
Post a Comment