Maswali ya TEHAMA ngazi ya certificate

  1. Eleza kwa kifupi maana ya neno `Mawasiliano`.
  2. Eleza madhara matatu ya kutosikia vizuri kwa mwanafunzi.
  3. Eleza matumizi ya vifaa vifuatavyokatika Kompyuta;
  • Kichakata Kikuu (KIKU).
  • Kibao Vifungo (KIBODI)
  1. Eleza kwa kifupi sifa nne za zana za kufundishia na kujifunzia somo la TEHAMA.
  2. Bainisha matumizi ya maneno yafuatayo katika muhtasari wa somo la TEHAMA.
  • Kiongozi cha Mwalimu.
  • Kitabu cha rejea.
  1. Orodhesha faida tano (5) za tathmini tamati.
  2. Taja tofauti Tatu (3) za majarida na magazeti.
  3. Toa maelezo mafupi kuhusu faida nne za maktaba katika jamii na Taasisi za kielimu.
  4. (a)   Eleza maana ya kufaragua zana za kufundishia na kujifunzia.

(b)Eleza faida tatu za kufaragua na kutengeneza zana za kufundishia na kujifunzia.

  1. Ni vifaa gani vya kimtaala anavyohitaji mwalimu kwa ajili ya kujiandaa katika ufundishaji wa somo la TEHAMA


  2. . Fafanua vigezo vitano vinavyoweza kutumika kuangalia uwezo wa mwalimu mwanafunzi wakati wa kufundisha somo la Mfano.

    12. Jadili umuhimu wa TEHAMA katika maisha ya watu kwenye jamii.

    13. Eleza maana ya vituo vya unasihi kisha fafanua faida nne za kuwa na vituo hivyo katika jamii.

    14. Jadili faida nne za umuhimu wa vyombo vya habari kwa nchi kama ya Tanzania.

    15. Eleza umuhimu wa mwalimu kutumia mbinu tofauti katika ufundishaji wa somo la TEHAMA.

    16. Andika barua ya kirafiki kwa kuzingatia mambo muhimu ya uandishi wa barua, ukimweleza rafiki yako jinsi unavyoendelea na masomo yako hapa Chuoni.

    17. (a) Eleza maana ya vituo vya Habari na Mawasiliano.

    (b) Kwa kutumia mifano eleza faida nne za matumizi ya vituo vya Habari na Mawasiliano.

    18. Eleza maana ya “Jedwali la Utaini” kisha bainisha ngazi zilizomo kwenye jedwali la utahini kwa kutoa swali moja kwa kila ngazi

     

Comments

Popular Posts

ZANA ZA KUFUNDISHIA NA KUJIFUNZIA

NUKUU ZA SOMO LA TEHAMA MWAKA WA PILI MEI 2020

Tathimini na Upimaji