JIPIME NA MASWALI YA UALIMU MWAKA WA KWANZA NA MWAKA WA PILI (Maswali na majibu)
Mei 2020
MAELEKEZO
Jaribu kujipima na haya maswali kidogo uuone ufahamu wako juu ya haya machache.
IMEANDALIWA MWALIMU ERICK GRATION
SEHEMU A
Taja sifa tano (5) za malengo mahususi. 2Marks@=10 marks
Fafanua dhana zifuatazo; 4marks@= 8 marks
Andalio la somo.
Azimio la kazi.
Ainisha misingi minne (4) katika uchaguzi wa maudhui ya mtaala. 2Marks@=8 marks
Taja umuhimu wa kujifunza makuzi ya mtoto. 6 marks
Kokotoa Hisa ya Akili ya Mwakayungu mwenye umri wa miaka 10 na anauwezo wa kufanya mambo ya mtoto wa miaka 15. 8 marks
Orodhesha sababu nne (4) za mtoto kuvia akili baada ya kuzaliwa. 2Marks@= 8marks
Toa tofauti iliyopo kati ya mtaala rasmi na mtaala usio rasmi. 8 marks
Taja mbinu tano (5) za ufundishaji kwa njia shirikishi. 10 marks
SEHEMU B 17 marks @
Eleza maana na umuhimu wa mazoezi ya kufundisha.
Jadili mbinu za kuzingatia katika utoaji wa ushauri nasaha.
“Mwalimu anaweza kuwa chanzo cha utovu wa nidhamu ya mwanafunzi.”. Fafanua kwa kutoa mifano kuhusu usemi huu.
Kuna haja gani ya kuhakiki mazoezi ya kufundisha kwa muda mrefu.
MWONGOZO WA USAHIHISHAJI SOMO LA UALIMU MWAKA WA KWANZA 2020
1. Sifa za malengo mahususi
I.lazima malengo mahususi yaandikwe katika hali ambayo n mahususi kwa kutumia kitenzi cha kutenda.
Malengo mahususi yanapaswa kuzingatia mwanafunzi kama mtendaji mkuu.
Malengo mahususi lazima yawe yanapimika.
Malengo mahususi lazima yaonyeshe ni kwa muda gani mafiliko la kitabia litatokea.
Malengo mahususi yabainishe ni maudhui gani mwanafunzi anatakiwa awe amejifunza na kwa kiwango kipi baada ya somo kufundishwa.
2.a. Andalio la somo
Andalio la somo ni utaratibu au mpangilio wa hatua za kufundishia unaotayarishwa na mwalimu kwa kipindi husika na kwa darasa husika. Andalio la somo ni dira ya kumuongoza mwalimu wakati anapofundisha.
b. Azimio la kazi.
Azimio la kazi ni mpangilio au utaratibu unaowezesha mwalimu kuchanganua muhtasari wa somo na kupanga mada na jinsi atakavyozifundisha katika kipindi cha wiki, mwezi na muhula.
Misingi ya uchaguzi wa maudhui ya mtaala
I.Uthabiti
ii.umuhimu
iii.Mvuto
iv.Kufundishika
4.Umuhimu wa kkujifunza makuzi ya mtoto.
Kuelewa kama mtoto anakuwa kulingana na hatua zote za kimakuzi.
Kutambua watotowenye mahitaji maalumu ili waweze kusaidiwa.
Kuweza kutoa mafunzo yanayoendana na umriwa mtoto.
Kuwapa watoto mahitaji yao ya kimsingi kulingana na kiwango chao cha kimakuzi.
Mwalimu kuweza kujitambua na kujitathmini katika tendo la ufundishaji.
Kutafuta hisa ya akili.
Taarifa tulizopewa.
Umri wa kuzaliwa = 10
Umri wa akilli = 15
Kinachohitajika = hisa ya akilli.
Njia.
Hisa ya akili = umri wa akili X 100%
umri wa kuzaliwa.
=15/10 X100%
=150%
Hiasa ya akili ya Mwakayungu = 150%
Sababu nne za mtoto kuvia akili baada ya kuzaliwa
Magonjwa mbalimbali kama malaria .
Ajali mbalimbali zinazoweza kuathiri ubongo.
Mtoto kukosa hewa ya oksijeni wakati wa kuzaliwa.
Athari za mazingira.
Tofauti kati ya mtaala rasmi na usio rasmi.
Mtaala rasmi huonyesha aina mbalimbali za masomo yatakayofundishwa
Hufundishwa kwa muda maalumu wakati mtaala usio rasmi hauna muda maalumu.
Mtaala rasmi huweka bayana utaratibu wa kutahini na sifa za wale watakaofuzu.
Mtaala rasmi hufundishwa katika utaratibu maalumu yaani mfumo rasmi kama vile shule,vyuo, taasisi wakati mtaala usio rasmi hauna mfumo maalum.
Mbinu tano za ufundishaji kwa njia shirikishi.
Mbinu ya maonesho
Mbinu ya maswali na majibu
Majadiliano ya vikundi.
Mbinu za ziara.
Mbinu ya kazi mradi (projekti)
Mbinu ya kutatua matatizo
Mbinu ya bunga-bongo
Mbinu ya majaribio
Mazoezi ya kufundisha ni hali ya mwalimu mwanafunzi kuweka taaluma ya kufundisha alioipata darasani katika hali ya kutenda.Hivyo mwanachuo ataandaa somo na kulifundisha kama anavyofanya mwalimu darsani.
Umuhinu wa mzoezi ya kufundisha
I.Humuwezesha mwalimu mwanafunzi kuunganisha taaluma ya darasani na vitendo.
ii.Kumpa mwalimu mwanafunzi uwezo wa kujiamini na kuelewa zaidi kilichofundishwa darasani.
Iii. Kumweka mwalimu mwanafunzi katika mazingira ya kupambana na kuyatatua matatizo yanayoweza kujitokeza katika mazingira ya kazi.
10. Mbinu za kuzingatia katika utoaji wa ushuri nasaha.
MBINU ZA KUNASIHI
Zifuatazo ni njia muhimu za kutolea Nasaha.
Mshauriwa kama kiini cha Nasaha.
Mshauri kama kiini cha Nasaha.
Eclectic Counseling.(Mbinu mseto)
Mshauriwa kama kiini cha nasaha
Lazima Mshauriwa ajisikie analo tatizo halafu amwendee mshauri kwa hiari yake ili apate ushauri wake.
Mshauri kama kiini cha nasaha
Mshauriwa siyo lazima ahisi kuwa ana tatizo , pia uamuzi wa kwenda kumuona Mshauri siyo lazima uwe wa mashauriwa mwenyewe. Tatizo linaweza likahisiwa na mshauri au mtu mwengine ambaye siyo Mshauriwa.
Mwallimu anaweza kuwa chanzo cha utovu wa nidhamu darasani kwa sababu zifuatazo.
I.Matumizi ya lugha chafu.
ii.Haiba mbaya..
Matumizi mabovu ya njia na mbinu za kufundishia.
Kutotumia zana au vifaa vya kufundishia
Uwezo wa mwalimu kuwa mdogo.
Utangulizi mbya wa somo
Sauti ya mwalimu
Kutofuata kanuni za ufundishaji
Mahusiano mabaya na wanafunzi
Kwa mwalimu wa mafunzo ya ualimu ni muhimu sana kufanya mazoezi ya kufundisha kwa muda mrefu. Mazoezi haya yanahakikiwa ili;
Kusadiwa kuelewa nafasi au uwezo wako wa kutenda kazi ya ualimu.
Kuelewa jinsi hali ya ufundishaji inavyokwenda
Kuweza kupima ubora na changamoto ya mtaala pamoja na mfumo wa elimu nchini.
Kubainisha maeneo unayohitaji msaada zaidi.
Comments
Post a Comment