Jipime na Maswali 50 ya TEHAMA
- Mbinu za kufundishia ni nini?
- Elimu ya awali ni nini?
- Eleza umuhimu na mapungufu ya Mtaala wa elimu Tanzania.
- Bainisha misingi ya kufanya upimaji wa kielimu
- Bainisha misingi ya kufanya tathmini ya mtaala
- Dhana ya lugha hujipambanua katika sura kuu tano. Taja sura kuu nne za lugha.
- Utajuaje kuwa tendo la kujifunza limekamilika kwa mwanafunzi wako?
- Kuna aina ngapi za unasihi?
- Taja stadi za kimaadili ambazo mwalimu huzijumuisha katika upimaji wa elimu.
- Je, kuna umuhimu gani wa mpango wa elimu hapa Tanzania?
- Onesha utaratibu wa uendeshaji wa elimu nchini Tanzania kwa mujibu wa sera ya elimu na mafunzo ya mwaka 1995.
- Je, umewahi kuuona mtaala wa shule ya msingi? Kama siyo kuna dosari gani ya kutouona mtaala huo?
- Tofautisha kati ya Utawala na Uongozi.
- Kwa kutumia mchoro onesha mtiririko wa Muundo wa uongozi chuoni.
- Nini maana ya Elimu ya watu wazima?
- TEHAMA ni nini?
- Fafanua dhana ya kusoma na kuandika.
- Eleza kwa kifupi maana ya Kisomo Chenye Manufaa (KCM) na Kisomo cha Kujiendeleza (KCK).
- Mwanafunzi mtu mzima ni nani?
- Fafanua dhana ya Elimu.
- Kujifunza kwenye maana kuna maana gani?
- Kwa kutumia mifano mitatu eleza maana ya kujifunza kipurure.
- Eleza kwa maneno yako mwenyewe maana ya “Uhawilishaji wa Maarifa”.
- Eleza kwa kutoa mifano maana ya uhawilishaji ulalo na uhawilishaji wima.
- Kuvia akili ni nini?
- Eleza mahitaji ya mwanafunzi katika umri wa kuanzia miaka 7 – 15.
- Kwa nini mwanafunzi hufundishwa stadi ya kuzungumza kabla ya kumfundisha stadi ya kuandika?
- Maarifa ni nini?
- Eleza na fafanua nadharia ya “Umwenendo”.
- Eleza maana ya usemi huu, “Motisho huongeza tija”.
- Nini umuhimu wa Elimu ya Maadili katika kujifunza?
- Kichocheo hasi hutolewaje?
- Kuna aina ngapi za motisho?
- Taja mambo yanayoonesha kuwa mwanafunzi amejifunza.
- Kuna manufaa gani kwa mwalimu kuwapa wanafunzi kazi za kufanya nyumbani?
- Eleza na fafanua misingi inayotumiwa wakati wa kutoa mazoezi.
- Tunga maswali matano (5) yanayopima ngazi ya juu ya maarifa.
- Taja aina tano (5) za zana unazoweza kutengeneza kutoka mazingira ya shule.
- Eleza manufaa ya kutumia zana wakati wa kufundisha.
- Taja na eleza aina mbalimbali za mbao za kufundishia.
- Eleza maana ya dhana. Toa mifano kusaidia ufafanuzi wako.
- Eleza hatua za kufuata wakati unapotaka kutatua tatizo lolote.
- Ubora wa njia yeyote unategemea mambo gani?
- Mwanafunzi anaweza kujifunza bila kuwapo kwa mwalimu. Eleza ni katika mazingira gani hali hii inaweza kutokea.
- Kwa mujibu wa Hurlock michezo ni nini?
- Jadili hitilafu tatu (3) za kuzungumza wanazopata watoto.
- Eleza kwa kifupi kuhusu mitihani ya insha.
- Eleza majukumu manne (4) ya Tume ya Utumishi ya Walimu (TSC).
- Taja faida tano (5) za maswali yanayoulizwa na mwalimu darasani.
- Kujifunza huimarika kwa kuzingatia Nyanja kuu tatu (3), zitaje.
Comments
Post a Comment