Dondoo za maisha

DONDOO ZA MAISHA: ISHI MAISHA YA FURAHA, PENGINE ULIPO SASA NDIO MBINGUNI YAKO

Duniani, kila saa, dakika au sekundi inapopitia kuna mambo mazuri yanatendeka. Hii inamaamisha dunia ndio sehemu pekee kuwahi kuona tukifurahia maisha.

Kama utakuwa makini, utaliona hilo. Kama utakuwa tayari, utasaidia kuendeleza hilo. Hebu tuchukue muda kutafakari ni mazuri mangapi yanatokea katika mazingira yetu.

Sasa hivi, wakati huu...
1. Kichanga kinavuta pumzi kwa mara ya kwanza baada ya kuzaliwa.
2. Wafanyakazi wawili wanakumbatiana na kucheka kwa nguvu kama hakuna anayewasikia.
3. Mlevi aliyesumbuka kuacha pombe kwa kipindi kirefu baada ya kupoteza dira ya maisha leo hatimaye anafurahi ameacha.
4. Mume na Mke wanafurahi hatimaye wamemaliza deni walilokuwa wanadaiwa na benki kwa kipindi cha miaka 10.
5. Mtu aliyekuwa na uzito kupindukia hatimaye anafu
ahi kwa kuwa amefikia malengo kwa kupunguza uzito alioshauriwa na daktari.
6. Marafiki wawili wanakumbatiana baada ya kutoonana kwa kipindi kirefu.
7. Mtu aliyekuwa anaumwa sana kwa muda mrefu sasa amepata nafuu anafanya shuguli zake kama kawaida.
8. Mtu anayofuraha amepata kazi ya ndoto zake baada ya kutafuta kazi kwa zaidi ya miaka 2.
9. Mtu anafurahi baada ya kutoka kupima VVU na vipimo vinaonyesha yupo salama baada ya kufanya ngono zembe mara nyingi sana.
10. Mtu anatabasamu kugundua kuwa maisha yake yapo mikononi mwake.

Hii inamaanisha furaha ndio kila kitu katika maisha, na ni wajibu wetu kuitafuta.
Na erick gration

Comments

Popular Posts

ZANA ZA KUFUNDISHIA NA KUJIFUNZIA

NUKUU ZA SOMO LA TEHAMA MWAKA WA PILI MEI 2020

MFUMO WA MMENG'ENYO WA CHAKULA