DONDOO ZA MAISHA YA KILA SIKU
May 2020
MAHUSIANO YAKO YANACHANGIA MAFANIKIO YAKO.
Mahusiano ni muhimu sana kwa maisha yetu, mahusiano yanauwezo wa kukujenga au kukupoteza kabisa mahusiano mengi ya kwetu hua yanatuonyesha na kutuinua kutoka sehemu moja kwenda nyingine.Ni muhimu sana kua na mahusiano ambayo yanatujenga na kutusogeza, kua na watu watu ambao wanaona ile ndoto iliyoko ndani yako, watu wanaofahamu unafanya nini na wanakusupport kwa kila hatua unayopiga, kukuamsha kila siku Asubuhi na kukumbusha kufanyia kazi ndoto zako.
Tunahitaji marafiki ambao wanafahamu kitu gani ni bora kwako na ndoto zako ni zipi na wakati mwingine kukupa ata mwangaza na njia za wewe kufika hapo ulipo, marafiki ambao unaweza kuamka asubuhi au usiku wa manane watapokea simu na kusikilza shida yako na kama kuna namna ya kukusaidia watafanya ivyo bila kuomba samahani/Hudhuru kwa kutokufanya yale ambayo unayotaka wakusaidie
AINA YA MARAFIKI WANAOJENGA.
- RAFIKI AMBAE ANA MTAZAMO CHANYA.
Tuna marafiki wengi sana na mitazamo yetu na yao ni muhimu kufanana ili kuweza kufanya kazi au kuendana katika mambo mengi,tunahitaji watu ambao watu wanamitazamo chanya kwenye kila kitu na watu ambao wana mbinu mbadala kila wakati ili kutukomboa kwa kila hali tunazokutana nazo kila wakati.Kufahamu na kuambiwa shida haitakiwi kukaa na kua na matazamo hasi katika hilo tatizo ila kua chanya na kua na mbinu ya kulikabili hilo tatizo wakati linapokuja na sio tu katika tatizo hata mipango yako atakua mstari wa mbele kukushawishi kujaribu maana anaelewa
- RAFIKI MKWELI.
Ukweli humfanya mtu kua huru pamoja na kwamba ukweli ni mchungu na mara nyingi hauonekani kama ni mzuri kwetu lakini tunauuhitaji na ukweli na kuna wakati ni mzito lakini hutusaidia kufika kwenye sehemu tunayohitaji Kufika na rafiki Mkweli hukufanya wewe kujifahamu na kufikia Malengo yako maana utafahamu sehemu gani unahitaji marekebisho sehemu gani unahitaji kubadilika na sehemu gani uongeze juhudi zaidi, Sisi hatujioni na hatuwezi tukajisemea na kufanya vitu vyetu lakini tunahitaji marafiki ambao watatushika mkono na kutueleza ukweli bila kujali wanatuumiza lakini pia kwa kuokoa nafsi zetu na malengo yetu.
- RAFIKI MWENYE KUFARIJI/KUTIA MOYO.
Tunapigana sana katika maisha na tunaaguka mara nyingi na tunahitaji watu wa kutuinua tena sio kwa kutupa fedha wala magari bali kutufariji na kufanya mioyo yetu kupiga tena ,Rafiki mwenye kutia moyo ni mali na thamani na anapaswa kulindwa,Tunafahamu kua pengine na yeye ana mambo yake mengi tu lakini kuamua kukusikiliza na kukufariji ni zawadi kubwa sana zaidi ya kukupa gari au fedha,Usimwache rafiki wa namna hii maana uyu ndie atakusuport katika kitu chako kwa maana furaha yako ni yake na hayupo tayari kuipoteza kwa namna yoyote ile.
Mithali 27;9,19
Marhamu na manukato hufurahisha moyo,Kadhalika utamu wa rafiki ya mtu utokao katika kusudi la moyo wa mtu.
19;Kama ufananavyo na uso katika maji ;Kadhalika moyo wa mtu na mwenzake.
Comments
Post a Comment