Mfumo wa Mmeng'enyo wa Chakula wa Binadamu Tafsiri: utumbo mwembamba (small intestine), utumbo mpana (large intestine), ini (liver), kongosho (pancrease), ulimi (tongue), tumbo (stomach), tezi za mate (salivary glands), umio (esophagus), puru (rectum), mkundu (anus) Mfumo wa mmeng'enyo wa chakula (pia: mwanya wa chakula [1] ) ni jumla ya viungo mwilini mwa binadamu na mamalia wengine vinavyofanya kazi ya kuingiza chakula mwilini, kukisagasaga, kukisafirisha ndani ya mwili, kukimeng'enya, kuondoa lishe ya mwili ndani yake, na kutoa mabaki nje ya mwili. Kwa hiyo mfumo wa mmeng'enyo wa chakula ni njia yote kuanzia mdomo hadi mkundu . Magonjwa yake huchunguzwa na elimu ya gastro-enterolojia . Kwa lugha nyingine unahusika na umeng'enyaji wa chakula mpaka kuwa katika hali inayoweza kusharabiwa na mwili. Ili chakula kiweze kutumika mwilini, ni lazima kivunjwevunjwe kiwe katika hali rahisi ya kuweza kusharabiwa. Kazi hiyo hufanywa ...
Comments
Post a Comment